Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi amewahimiza wakaazi wa Malindi na kaunti ya Kilifi kwa ujumla kujitokeza ili kushiriki kwenye zoezi la sensa.
Akihutubia wakaazi wa Malindi baada ya ufunguzi rasmi wa soko la kwa Jiwa mjini Malindi, Gavana Kingi amesema zoezi hilo ni muhimu na hakuna wananchi anayepaswa kulipuuzilia.
Gavana Kingi amehoji kuwa mipangilio ya nchi yaiwezi kuendelea iwapo serikali haitajua idadi kamili ya wananchi wake.
Wakati uo huo amedai kuwa kuna baadhi ya maafisa ambao wametishia kutoshiriki zoezi hilo kutokana na madai kuwa hajalipwa marupurupu yao, akitaka swala hilo kushuhulikiwe ili kuzuia sintofahamu.
Taarifa na Charo Banda.