Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho ameonekana kuunga mkono azma ya Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ya kuwania ugavana wa Kaunti hiyo.
Katika matamshi yake ya hivi punde, Joho ameonekana kumpendekeza Nassir kumrithi katika kinyang’anyiro cha Ugavana wa Kaunti ya Mombasa katika uchaguzi wa mwaka wa 2022.
Kwa upande wake, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amewarai Wakaazi kumuunga mkono katika azma yake ya kuunyakua ugavana wa Kaunti hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Nassir hata hivyo amewaonya wanasiasa dhidi ya kueneza siasa za ukabila na mgawanyiko miongoni mwa wakaazi wa Kaunti ya Mombasa.
Kipute hicho cha ugavana wa Kaunti ya Mombasa kimewavutia wengi akiwemo Mfanyibiashara Suleiman Shahbal, Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo, Spika wa bunge la Kaunti ya Mombasa Aharub Khatri miongoni mwa wagombea wengine.