Picha kwa hisani –
Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amewatahadharisha wakaazi wa Kaunti hiyo dhidi ya kupuuza masharti ya kiafya ya kujikinga na virusi vya Corona.
Joho amesema janga la Corona limeashiria makali yake zaidi akisema ni jukumu la wakaazi kujikinga wenyewe na wala sio kupotoka kimaadili na kusubiri kulazimishwa kuzingatia masharti ya afya.
Wakati uo huo, Joho amesema serikali yake inaendeleza mikakati ya kuzuia maambukizi miongoni mwa Wakaazi akisisitiza ni sharti wakaazi wenyewe wajikinge na virusi hvyo.
JOHO – MIKAKATI 21 10 20