Story by Gabriel Mwaganjoni –
Gavana wa kaunti ya Tana River Meja mstaafu Dhadho Godhana amedhihirisha wasiwasi wake kuhusu mgawanyiko na chuki za kikabila zinazoshuhudiwa katika kaunti ya Tana river.
Gavana Dhadho amesema chuki hizo zimeathiri hadi shughuli mbalimbali za kiserikali huku serikali ya kaunti na maafisa wa serikali ya kitaifa wakitengana na kukosa kufanya kazi kwa pamoja.
Akizungumza katika kaunti ya Tana river, Dhadho amesema hali hiyo imedunisha maswala ya amani na usalama pamoja na mambo ya kiuchumi huku akiwasihi viongozi na wasimamizi wa Idara mbalimbali za Serikali ya kaunti hiyo na ile ya kitaifa kushirikiana.
Dhadho amehoji kwamba baadhi ya maafisa wa serikali ya kitaifa wamedinda kuhudhuria makongamano muhimu ya kujadili maendeleo, uchumi, elimu, usalama na amani katika kaunti hiyo, hali inayoathiri mshikamano wa kijamii.
Kiongozi huyo amesema hali hiyo kwa sasa imedhihirika wazi katika bunge la kaunti hiyo ambapo wajumbe na maafisa wengine wamekuwa wakilumbana bungeni bila ya kuangazia miswada muhimu ya kuwajenga kimaisha wakaazi wa kaunti hiyo.