Story by Our Correspondents-
Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema serikali imejitolea kikamilifu kusaidia idara ya usalama nchini kuhakikisha inawajibikia majukumu yake kwa wananchi.
Akizungumza jijini Nairobi, Gachagua amesema juhudi hizo zitachangia mazingira bora ya kikazi kwa maafisa wa usalama, akisisitiza haja ya maafisa wote wa usalama nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingitia sheria.
Naye Waziri wa usalama nchini Prof Kithure Kindiki amewarai viongozi wa kidini kuendelea kuwaunga mkono maafisa wa polisi pamoja na familia zao katika imani ili kutekeleza majukumu ya kiusalama waliokula kiapo.
Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki jimbo la Nairobi Philip Anyolo amewasihi wakenya kushirikiana na maafisa wa usalama ili kuhakikisha usalama wa taifa unaimarishwa.