Story by: Charo Banda
Serikali ya kaunti ya Kilifi imeweka wazi kuwa bado elimu katika kaunti hiyo haijafikia viwango hitajika.
Naibu Gavana wa Kilifi, Flora Chibule amesema japo serikali ya kaunti ya Kilifi imepiga hatua kuhakikisha sekta ya elimu ya chekechea inaboreshwa bado juhudi zaidi zinahitajika.
Chibule ametaja swala la umaskini, baa la njaa na muundo msing duni katika taasisi nyingi za kielimu kaunti ya Kilifi kama mojawapo ya changamoto zinazochangia kuzorota kwa sekta ya elimu.
Wakati uo huo amesema swala la mimba za utotoni katika kaunti hiyo limechangiwa na watu wa karibu wa familia ya muathiriwa, akisema ni lazima jamii ijitenga na hulka hiyo ndipo mtoto wa kike atatimiza ndoto yake.