Story by Mercy Tumaini-
Mgombea mwenza wa Gedion Mung’aro wa ugavana wa kaunti ya Kilifi kwa tiketi ya chama cha ODM Flora Chibule Tsuma amehimiza ushirikiano wa jamii na viongozi wengine ili kufanikisha maendeleo ya gatuzi la Kilifi.
Flora amesisitiza umuhimu wa wananchi kuzingatia mafunzo ya mwenyezi Mungu na kujitenga na maswala potovu ambayo huenda ya kavuruga maandalizi ya uchaguzi mkuu.
Flora aidha ameahidi kuhakikisha uongozi wa serikali itakayobuniwa na kiongozi wake Gideon Mung’aro inawashirikisha viongozi wote katika kaunti hiyo ikiwemo wale wa kidini na wadau wengine.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Rabai Pastors Fellowship Mchungaji Lennox Kalu amesisitiza umuhimu wa wanasiasa kuzingatia siasa za amani huku akidai kwamba kama kanisa watashirikiana na kiongozi atakayechaguliwa na wananchi.