Taarifa na Charo Banda
Malindi, Kenya, Julai 12 – Kama njia moja wapo ya kuboresha sekta ya utalii kanda ya Pwani sasa serikali kupitia shirika la huduma za ferry katika kivuko cha Likoni sasa limeweka wazi kwamba feri zote za zamani zitageuzwa kuwa hoteli zinazoolea baharini.
Kulingana na Mkurugenzi wa shirika la feri , Bakari Hamisi serikali kupitia shirika hilo inapania kuwekeza katika hoteli za kuolea baharini wakitumia feri za zamani kama mbinu ya kuleta mapato kwenye shirika hilo.
Kando na hayo feri hizo zitatumika kama makavazi ya kitaifa na kutumika kama vivutio kwa watalii ambapo watalii watakuwa na uwezo wa kufurahia mandhari ya bahari kutumia feri hizo kutoka Mombasa kuelekea Lamu.
Mkurugenzi huyo, amesema haya kwenye washa moja iliyowajumuisha wanachama wote wa bodi hiyo ya feri inayoelendea kwa siku ya pili katika hoteli moja mjini Malindi.