Picha kwa hisani –
Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha ametoa hakikisho kwamba tayari shilingi bilioni 4 za kugharamia mpango wa elimu ya bure ya shule za msingi zimesambazwa katika shule zote za msingi za umma nchini.
Akizungumza baada ya kuzuru shule moja ya mabanda katika kaunti ya Nyeri Magoha amesema shilingi bilioni 14.6 za kugharamia masomo ya shule za upili zilizopangwa kutumwa katika shule hizo siku ya ijumaa tayari zimesambazwa katika shule hizo.
Magoha ametangaza kwamba wakati huu ambapo masomo yamerejelewa rasmi atazuru shule zote za mabanda nchini ili kukagua mazingira ya shule hizo kuhakikisha usalama wa wanafunzi unazingatiwa.
Magoha amewataka wazazi kuwaripoti mara moja waalimu wanaowarejesha nyumbani wanafunzi kwa ajili ya fedha za maendeleo na kwamba wizara ya elimu itachukua hatua za kuwakabili waalimu hao.