Picha Kwa Hisani –
Aliyekuwa mpenzi na mzazi mwenza wa Rayvanny, Fahyma ameshindwa kuvumilia maumivu ya mapenzi na kuamua kumzomea mpenzi huyo wake wa zamani kupitia mtandao wa Instagram.
Kwa muda sasa, kumekuwa na zogo kati ya Rayvanny na mwanamuziki Harmonize kuhusu msichana kwa jina Paula mtoto wa Frida Kajala na mengi yameanikwa kwenye mitandao.
Fahyma ambaye hujiita Fahyvanny kwenye mitandao huo sasa analalamika akisema Rayvanny ameaibisha familia yake na amechoka kufanywa mjinga.
Wengi wanafahamu kwamba wawili hao walitengana ila wanasaidiana katika malezi isijulikane ni kwa nini Fahyma amemrejelea Rayvanny kama familia.
Picha Kwa Hisani –
Kupitia Instagram stories bila kutaja jina, Fahyma ameandika maneno haya; “Unashindwa kuilinda familia yako na mambo mabaya, ila kila siku wewe umekuwa mstari wa mbele kutudhalilisha kwenye jamii. Unasahau una mtoto ambaye anasoma. Kule shule anaposoma atawaangaliaje watoto wenzake wenye familia zinazojiheshimu? Wewe umekuwa mstari wa mbele kuleta maumivu na fedheha kwenye nyumba yako. Endelea kuwa huru maana huu ujinga mimi sitaki tena’’.
Picha Kwa Hisani –
Mwezi Januari mwaka huu, Fahyma alichapisha picha ya Rayvanny kwenye Instagram na kumrejelea kama mume wake katika hatua labda ya kutangaza kwamba wamerudiana lakini Rayvanny alimshurutisha kupitia ujumbe kwenye picha hiyo kuwa aifuta haraka.