Picha Kwa Hisani –
Mwanamitindo, mfanyibiashara na video vixen kutoka Tanzania, Fayhma amekana madai ya kukerwa na mahaba kati ya Nana na baba mtoto wake, Rayvanny na kumsababisha kutoroka kwenye ukumbi wa kutumbuizwa kwenye harusi ya Esma Platnumz. Hii ni baada ya tetesi kuenea kuwa Fayhma aliguswa na nyimbo iliokuwa ina imbwa na Rayvanny na mahaba aliokuwa anamuonyesha Nana ukumbini, kitu kilicho mkera Fayma.
Kwenye video moja iliyochukuliwa ukumbini Fayhma, mama Jaydan, akitoka ukumbini kwa kasi kuelekea alipokuwa ameegesha gari. Tetesi za uhusiano wa Nana na Rayvanny zilianza baada ya kutokea kwenye video ya ‘I love you’ na kudaiwa kutembea kimapenzi na Rayvanny, kitu ambacho kilichangia kuvunjika kwa ndoa ya Fayhma na Rayvanny. Tetesi hizo pia zinadai kuwa mtoto wa Nana aliyezaliwa miezi michache iliyopita ni wa rayvanny ingawaje wahusika wenyewe wamekana madai hayo.
Kupitia kituo kimoja cha habri mijini Dar Es Salaam, Fayhma amekanusha madai hayo akisema kwamba alikuwa amechoka na kwa kuwa sherehe hiyo ilikuwa inaelekea kufika tamati akaona heri kutangulia kwa gari ili aepuke mahojiano na wanahabari. Fayhma pia alikanusha kuwa Rayvanny yupo katika mahusiano ya kimapenzi na Nana na kueleza kuwa hahusiki na matatizo anayo yapitia kwa ndoa yake.
“Hahusiki na kitu chochote kile na nahisi kuwa watu wanamuonea dada wa watu. Je, ningewaeleza kuwa mimi ndio nlitoka na Rayvanny ukumbini? So sitaki kuzungumzia ndoa yangu na Rayvanny…” – Fayhma
Je, una matumaini kuwa penzi la Rayvanny na Fayma litaregea kama zamani?