Zaidi ya familia 40 zilizoathirika na mafuriko katika eneo la Lasco-Ziwani Kisiwani Mombasa sasa wanaitaka Serikali ya Kaunti hiyo kuwajumuisha kwenye mpango wa ugavi wa chakula cha msaada.
Kulingana na waathiriiwa hao,serikali ya Kaunti hiyo imekuwa ikiendeleza ugavi wa chakula hicho cha msaada lakini bado haijawaangazia wale wanaohitaji zaidi msaada huo.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Benjamin Mzungu Rocha, Wakaazi hao wamesema wameathirika zaidi kwani shughuli zao ndogo ndogo za kiuchumi zimesitishwa kutokana na athari za virusi vya Corona.
Rocha ameisihi Serikali ya Kaunti ya Mombasa kuwasajili wakaazi wa mitaa ya vitongoji duni kwa chakula hicho cha msaada.