Mwanaharakati wa maswala ya kijamii jijini Mombasa Lubinah Nassir Muhdhar anaitaka serikali kuu kupitia idara ya usajili wa watu nchini, kuzipa vitambulisho vya kitaifa familia zinazoishi barabarani katika kaunti ya Mombasa.
Kwa mujibu wa Bi. Muhdhar, stakabadhi hiyo muhimu itawezesha familia hizo kutambulika kama wakenya na kunufaika na huduma mbali mbali za serikali, mbali na kuepuka dhulma nyingi wanazopitia kwa kukosa vitambulisho vya kitaifa.
Ameihimiza jamii kutowabagua vijana wanaorandaranda mitaani na badala yake iwasaidie kujinasua kutoka kwenye maisha hayo.
Taarifa Na Hussein Mdune