Mjane wa mtangazaji Ahmed Darwesh, Hawa Hussein aliponea chupuchupu pale majambazi walipomvamia nyumbani kwake Kitengela, Jijini Nairobi.
Majambazi waliokuwa wamejihami walivamia nyumba hiyo ambapo Hawa anaishi na binti yake.
Kulingana na Hawa majambazi hao walimshinda nguvu mlinzi kabla ya kuingia kwenye nyumba.
Hawa amesema kuwa alichapwa na upande wa upanga mara kadhaa.
Wezi hao waliiba vitumeme, kapeti, patipati na vitu vingene walivyoweza kubeba kwa urahisi.
Taarifa na Dominick Mwambui.