Zaidi ya famila 3,000 zilizoathirika na mafuriko katika maeneo ya Malindi na Magarini kaunti ya Kilifi, zimenufaika na ufadhili wa mbegu na vifaa vya kilimo kwa gharama ya shilingi milioni 8.
Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amesema maafisa wa kilimo watakwenda nyanjani kuwapa wakulima mafunzo ya jinsi ya kutunza mimea yao ili kuzalisha mazao bora.
Gavana Kingi amesema mbali na mbegu hizo, serikali ya kaunti ya Kilifi pia ina mikakati ya kuwawezesha wakulima wanaoshi kando kando ya mito kuanzisha Kilimo cha unyunyizaji maji mashamba.
Taarifa na Marieta Anzazi