Familia 180 kutoka kaunti ya Kwale zitanufaika na msaada wa chakula kilichopeanwa kwa serikali ya kaunti hiyo kwa ufadhili wa benki ya KCB pamoja na wafanyibiashara wa mjini Kwale .
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo wa chakula waziri wa kilimo na mifugo kaunti hiyo Joan Nyamasio amesema msaada huo wa chakula utasaidia pakubwa familia zilizoathirika na janga la Corona.
Kwa upande msimamizi wa benki ya KCB mjini Kwale Jonathan Rono amesema chakula hicho kitasaidia wakaazi ambao kazi zao zimeathirika na janga la Corona
Benki hiyo imeweza kutoa bandali 80 za unga pamoja na mafuta ya kupikia lita 120 kwa famialia zilizoathirika .
Naye mwenyekiti wa wafanyibiashara Kwale Salim Mwayongwe amewataka wakaazi wa kwale kufuata kanuni za afya mbali na mikakati ya kupewa chakula .