Seneta wa Kaunti ya Mombasa Mohammed Faki amewataka viongozi wa kisisa nchi kujitenga na siasa za uchaguzi wa 2022 na badala yake kuwajibikia majukumu yao ya kiserikali.
Akiongea mjini mombasa faki amesema Hatua hii inatia aibu mno kwani amesema ni mapema mno kwa viongozi kuonyesha mivutano ya kisiasa kwani amesema wananchi wangali bado wanahitaji maendeleo.
Wakati uo huo Amesema wakati ni sasa viongozi kuangazi maswla ya kujenga taifa hili kiuchumi na biashara Bali simivutano na tamaa za uongozi.
Hata hivyo Amewataka viongozi kushirikiana na raisi uhuru kenyetta katiaka kuimarisha ajenda zake nne za kimaendeleo Bali sikukinzana nayee kisiasa.
Taarifa na Hussein Mdune.