Story by Our Correspondents –
Mamlaka ya kudhibiti Kawi na petroli nchini EPRA imeongeza bei ya mafuta kote nchini kwa shilingi 9.90 kwa lita kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Daniel Kiptoo amesema Mamlaka hiyo imezingatia sheria ya petroli ya mwaka wa 2019 sehemu ya 101 ambayo inaipa nguvu mamlaka hiyo kuongeza bei ya mafuta.
Kiptoo amesema changamoto zinazoshuhudiwa nchini hasa kwa mafuta zimechangiwa pakubwa na kupanda kwa mali ghafi kwa asilimia 14.2 tangu mwezi Machi mwaka huu na kufikia dola za Marekani 85.11 kwa lita.
Sasa Mafuta ya petroli nchini yatauzwa kwa shilingi 173.70 kwa lita, Mafuta ya Diseli yakiuzwa kwa shilingi 165.73 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa shilingi 139.89.