Picha kwa hisani –
Mchekeshaji na muigizaji maarufu mwenyewe umri wa miaka 10 nchini Nigeria, Emmanuela,
amefanikiwa kumjengea mama yake mzazi nyumba kama zawadi kupitia talanta yake.
Emanuella alipachika picha ya nyumba hiyo maridadi kwenye ukurasa wake wa Instagram na
kumshukuru mama yake kwa upendo na maombi yake kwake, ambayo anaamini ndio Siri ya mafanikio
yake.
Mchekeshaji huyo pia alifichua mipango yake ya kumjengea nyumba ingine kubwa zaidi na yenye
thamani ya juu zaidi. Mashabiki wake walimpa hongera kwa kumkumbuka mama yake baada ya
kufanikiwa maishani kutokana na talanta yake.