Story by Gabriel Mwaganjoni –
Maafisa wa polisi wanaosimamia mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE unaoendelea katika kaunti ya Mombasa wametakiwa kuwa makini na kutoruhusu wizi wa mtihani huo.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema ni lazima maafisa hao wawajibike katika kuhakikisha hakuna visa vyovyote vya wizi wa mtihani vinavyoshuhudiwa katika vituo vya mtihani katika kaunti hiyo.
Akizungumza katika gatuzi dogo la Jomvu aliposhuhudia usambazaji wa mtihani katika eneo hilo, Elungata ameseam maafisa hao watajipata matatani endapo watashirikiana na watu wengine katika kuiba mtihani huo.
Elungata ambaye alikuwa ameandamana na Kamanda mkuu wa polisi Pwani Manase Musyoka, Kamishna wa kaunti ya Mombasa Lucas Mwanza na Mkurugenzi mkuu wa elimu kaunti ya Mombasa Peter Magiri amesema juma la kwanza la mtihani huo uliyoanza siku ya Jumatatu halijakumbwa na utata wowote.