Story by Gabriel Mwaganjoni –
Machifu wote wanaoshirikiana na baadhi ya wafugaji ili kuwalisha mifugo wao kwenye mashamba ya wenyewe katika eneo la Tana delta watafutwa kazi.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema machifu hao wameshindwa kusaidia katika kudumisha uiano na amani na badala yake wamekuwa wakiwabaguwa watu wasiokuwa wa makabila yao.
Kulingana na Elungata, machifu hao wanapaswa kutekeleza majukumu yao akisema Chifu yeyote atakayezembea na kuchangia mizozo kati ya wakulima na wafugaji atapoteza kazi yake.
Elungata amesema ni sharti maafisa tawala katika kaunti ya Tana river kuwahudumia wakaazi bila ya ubaguzi, akiwataka kuhakikisha wale walioleta ng’ombe wao katika kaunti hiyo kuwarudisha mara moja kule walikotoka.