Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amewarai wakaazi wa kaunti ya Tana river kutopuuza masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Elungata amesema wakaazi wengi katika kaunti hiyo wamejitenga na kuvaa barakoa au kuweka umbali wa angalau mita moja katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza katika eneo la Odha huko Tana delta, Elungata amesema hali hiyo ni hatari kwani kaunti ya Tana river sawia na kaunti nyingine za Pwani zimeathirika pakubwa na janga la Corona.