Story by Gabriel Mwaganjoni-
Wakaazi walioyahama makao yao katika eneo la Lamu magharibi kufuatia msukosuko wa kiusalama wametakiwa kurudi majumbani mwao kwani usalama eneo hilo umeimarishwa.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema polisi wa akiba wamewekwa katika eneo hilo ili kupiga jeki juhudi za vitengo vingine vya usalama katika kuwalinda wananchi.
Akizungumza katika eneo la Kibaoni katika kaunti hiyo ya Lamu baada ya kufanya ziara ya kiusalama, Elungata amewataka wakaazi waliyokimbia makwao katika maeneo ya Hindi na Mpeketoni kufuatia utata huo wa kiusalama kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao bila ya hofu yoyote.
Wakati uo huo, ameitaka jamii ya eneo hilo kushirikiana na vitengo vya usalama ili kuyazima magenge la kihalifu au washirika wa mtandao wa kigaidi wa Al-shabab.
Kufikia sasa jumla ya watu 15 wameuwawa kinyama wakiwemo maafisa wa polisi, nyumba kadhaa kuchomwa huku mifugo wakiibwa.