Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Dongo Kundu inayounganisha kaunti za Mombasa na Kwale katika eneo la Bonje unaendelea vyema.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema mradi huo utabadili mbinu za uchukuzi na kumnufaisha mkaazi wa eneo la Pwani.
Akizungumza alipozuru mradi huo, Elungata amesema shughuli za ujenzi wa barabara hiyo zitapiga jeki uchumi wa ukanda wa Pwani, akiwasihi wakaazi wa eneo la Pwani kuikumbatia miradi hiyo ya Serikali.
Elungata hata hivyo amekiri kwamba utata kuhusu fidia unashughulikiwa na hivi karibuni wale waliyoathirika na mradi huo watafidiwa kikamilifu.