Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mradi wa ujenzi wa bwawa la maji la Mwache katika gatuzi dogo la Kinango kaunti ya Kwale utaanza kabla ya kukamilika kwa mwaka huu.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema kufikia sasa zaidi ya watu elfu 12 wameondolewa katika eneo litakalotekelezwa mradi huo hali iliyofikisha asilimia 78 ya familia ambazo tayari zimehama kutoa nafasi ya mradi huo.
Elungata amesema kufuatia kupatikana kwa nafasi hiyo, ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza wakati wowote kabla ya mwaka kukamilika akisema utasitisha uhaba wa maji katika kaunti za Mombasa na Kwale.
Elungata amesema mradi huo utatoa nafasi ya shughuli za kilimo cha kisasa cha unyunyizi maji mashamba katika eneo hilo.