Story by Gabriel Mwaganjoni-
Idara ya usalama katika kaunti ya Mombasa imeharamisha siasa za usiku katika kaunti hiyo.
Mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amewataka wanasiasa kuendeleza kampeni zao nyakati za mchana akisema siasa za usiku zimezua wasiwasi na hofu miongoni mwa wakaazi.
Akizungumza katika kikao cha kiusalama mjini Mombasa, Elungata amesema imekuwa vigumu kwa maafisa wa usalama kubainisha kati ya wahalifu na wafuasi wa wanasiasa wanaoendeleza kampeni zao nyakati za usiku.
Wakati uo huo Afisa huyo tawala ameharamisha hatua ya wanasiasa ya kubandika picha zao kwenye vyombo vya usafiri wa umma akisema hali hiyo huenda ikazua mtafaruku hasa kwa makundi pinzani akiwataka kubandika picha hizo kwenye magari yao pekee.