Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amewatahadharisha wale wanaondeleza maswala ya itikadi kali na uchochezi katika kaunti ya Tana river kwamba watakabiliwa kisheria.
Elungata amesema mara nyingi vurugu na msukosuko wa kiusalama katika kaunti hiyo huchangiwa na wanasiasa, akisema hali hiyo haitavumiliwa tena.
Akizungumza huko Tana delta, Elungata amesema hakuna mwanasiasa yeyote aliyepotoka kimaadili atakayeruhusiwa kuipotosha jamii ya kaunti hiyo hasa msimu huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Elungata amesema Serikali inafanya kazi na jamii mashinani ili kuhakikisha kuna usalama, amani na uiano katika kaunti ya Tana river.