Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amewaonya wakaazi wa kaunti ya Lamu dhidi ya kueneza chuki kupitia mitandao ya kijamii.
Elungata amesema hali hiyo imezua taharuki katika kaunti ya Lamu na kuwafanya baadhi ya wakaazi kutorokea msituni wakihofia kuvamiwa.
Elungata amesema japo msukosuko wa kiusalama katika kaunti hiyo ulisababisha jumla ya watu 15 kuuwawa kinyama wakiwemo maafisa 4 wa idara ya ulinzi nchini KDF, ni sharti semi hizo za chuki mitandaoni zikomeshwe.
Elungata amehimiza ushirikiano kati ya wakaazi na vitengo vya usalama ili kudhibiti msukosuko wa kiuhalifu katika kaunti hiyo.