Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema ujenzi wa kiwanda cha ndizi katika kaunti ya Taita taveta utasaidia pakubwa katika kilimo cha ndizi kinachoendelezwa katika maeneo la kaunti hiyo.
Elungata amesema licha ya wakulima wa ndizi kujitahidi kulikuza zao hilo, wamekosa soko, na kuitazama mali yao ikiharibika shambani.
Akizungumza alipozuru mradi wa kilimo wa ziwa chala kaunti ya Taita Taveta, Elungata amelitaka Shirika la ustawi wa ukanda wa Pwani la CDA kuhakikisha wakulima hao wa ndizi wanapata soko la mavuno yao kabla ya kukamilika kwa kiwanda cha ndizi katika kaunti hiyo.
Elungata amesema juhudi za wakulima hao haziwezi kupotea bure ilhali Shirika hilo lina uwezo wa kuwatafutia soko wakulima hao wa ndizi.