Story by Bakari Ali-
Jamii imehimizwa kushirikiana na idara ya usalama katika kuimarisha usalama badala ya kukejeli utendakazi wa idara hiyo.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema hatua hiyo itaboresha zaidi utendakazi wa idara ya usalama na kukabiliana kikamilifu na wahalifu.
Akizungumza katika eneo la kivuko cha feri cha Likoni kaunti ya Mombasa, Elungata amesema maafisa wa usalama wako macho kuhakikisha wanalinda maisha ya wananchi.
Wakati uo huo, amesema idara hiyo imeimarisha usalama wa kutosha katika ukanda wa Pwani kwani wanapania kuinua sekta ya utalii.