
????????????????????????????????????
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni
Mombasa. Kenya, Julai 17 – Hali ya vijana kujihusisha na maswala ya uhalifu, itikadi kali na utumizi wa dawa za kulevya katika Kaunti ya Mombasa umedidimiza viwango vya elimu katika Kaunti hiyo.
Afisa mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika Kaunti hiyo, Rajab Mohammed Said amesema kwamba hali hiyo ni ya kusikitisha mno kwani vijana hao hawajengi msingi wowote wa maisha yao ya sasa na ya mbeleni.
Akizungumza katika afisi za Shirika hilo mjini Mombasa hii leo, Rajab ameongeza kwamba bila ya maswala hayo kuangaziwa katika ngazi ya serikali na kuishirikisha moja kwa moja jamii mashinani, basi msingi wa elimu, jamii na uchumi wa kaunti hivyo vitadidimia.
Kulingana na Rajab, ni lazima kila mikakati kuwekezwa hasa ile ya kuwatumia Vijana katika kuwanasua Vijana wenzao kutoka kwa hali hiyo, ili kuwatenga Vijana na maovu na kuwafanya watu muhimu mno watakaoihudumia jamii vyema.