Picha kwa hisani –
Tume ya maadili na kupambana na ufisa nchini EACC inaendeleza hamasa kwa wawakilishi wadi katika kaunti zote 47 kuhusiana na maadili mema na uogozi.
Kamishna wa tume hio Rose Mghoi Macharia amesema EACC imechukua hatua hio kufuatia ongezeko la visa vya utovu wa maadili miongoni mwa wawakilishi wadi hasa wanapojadili miswada katika mabunge ya kaunti.
Bi Macharia amesema tayari wamewahamasisha wawakilishi wadi kutoka kaunti nne za humu nchini na juma hili wataendeleza hamasa hizo kwa wajumbe wa kaunti za pwani.
Amesema wanapanga kutoa mafunzo hayo kwa wawakilishi wadi wa kaunti zote 47 nchini ili kumaliza visa vya utovu wa maadili katika mabunge ya kaunti.