Picha kwa hisani –
Baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoegemea upande wa Naibu Rais Dkt William Ruto, wamejitokeza na kuwaonya vikali wanaopigia debe mchakato wa BBI dhidi ya kauli zao za kumdhalilisha Naibu rais.
Viongozi hao wakiongozwa na mbunge wa Garissa mjini Aden Duale, wamesema viongozi wanaopigia debe BBI wamekuwa wakiendeleza siasa za vitisho na madharau dhidi ya Naibu Rais, huku wengine wakipanga kuwasilisha hoja bungeni ya kumtimua mamlakani Ruto.
Wakizungumza kule Karen jijini Nairobi katika makaazi ya Ruto, Duale na wenzake wamesema wako tayari kuupiga na chini mswada huo iwapo utawaslishwa bungeni.
Mapema hii leo, Katibu mkuu wa Chama cha Jubilee Raphael Tuju, alipinga vikali kauli hizo, akisema chama cha Jubilee hakina nia yoyote ya kuwasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Ruto kwani chama hicho kinamtambua Ruto kama Naibu rais.
Kauli hizo zimejiri baada ya mbunge wa Lugare Ayub Savula, kumtaka Ruto kujiuzulu wadhfa wake wa Naibu Rais ama atawasilisha mswada bungeni wa kutokuwa na imani naye.