PICHA KWA HISANI
Maafisa wa polisi Kisiwani Mombasa wameirisha doria katika eneo Old town ili kuhakikisha wakaazi wanazingatia amri ya kuingia au kutoka katika eneo hilo.
Afisa mkuu wa polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Urban Eliud Monari amewaonya wakaazi wa eneo hilo dhidi ya kukiuka amri hiyo, akisema atakayenaswa atatiwa nguvuni na kuwekwa karantini kwa siku 14 kwa gharama yake mwenyewe.
Monari, amesema ni sharti amri hiyo izingatiwe kikamilifu na wakaazi kushirikiana na polisi ili kuhakikisha hakuna mvutano kati ya wakaazi na maafisa wa usalama.
Hata hivyo shughuli nyingi za kibiashara katka eneo hilo zimesalia kufungwa huku Shirika la kupambana na uraibu wa dawa za kulevya la ‘Reachout Centre Trust’ likiwa miongoni mwa walioathirika baada ya kulazimika kufunga shughuli zao zote.