Picha kwa hisani –
Waziri wa usalama wa ndani Dakta Fred Matiang’i amewahakikishia watumizi wa daraja jipya la Liwatoni kwamba wataongezewa usalama ili wavuke bila ya hofia.
Kulingana na Matiang’i, Idara ya usalama Kaunti ya Mombasa imepokea lalama kwamba baadhi ya Wakaazi wamehofia kutumia daraja hilo kutokana na hali ya usalama hasa katika eneo la Mtongwe.
Akizungumza alipokagua daraja hilo hapo jana, Matiang’i amesema mradi huo umesaidia kupunguza msongamano uliyokuwa ukishuhudiwa katika kivuko cha feri cha Likoni.
Amewataka wananchi wanaotumia daraja hilo kutoukosoa mradi huo akisema umekuja wakati mwafaka ambapo kivuko cha feri kimekuwa kikishuhudia msongamano na athari ya maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwa watumizi wa kivuko hicho.
Kulingana na Matiangi zaidi ya wakaazi elfu 20 wanatumia daraja hilo la Liwatoni kila siku.