Mbunge wa Msambweni katika kaunti ya Kwale Suleiman Dori ameihimiza jamii pwani kuungana kwa manufaa ya maendeleo.
Dori amewahimiza wanajamii kufanya maamuzi ya busara wakati wa kuchagua viongozi wao wakiongozwa na uwezo wa kiongozi kufanya maendeleo na wala sio misingi mingine yoyote.
Ameitahadharisha jamii dhidi ya kuongozwa na misingi ya vyama badala yake wachague kiongozi mchapa kazi ambaye atawaidhinishia miradi ya kimaendeleo itakayoleta manufaa kwa jamii.
Taarifa na Jumwa Mwandoro.