Story by Fatuma Rashid –
Mjumbe mpya wa Wadi ya Mahoo katika eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita taveta Donald Fundi Saleri ameapishwa rasmi kuchukua hatamu ya uongozi.
Saleri ameapigwa na Spika wa bunge la kaunti hiyo Meshack Maghanga katika halfa iliyofanyika katika majengo ya bunge la kaunti ya Taita taveta wakati wa kikao maalum.
Saleri ameapishwa baada ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 16 mwezi Disemba mwaka uliopita na kupata jumla ya kura 1,609 huku mpinzani wake wa karibu Daniel Kimuyu wa chama cha UDA akipata kura 1,358.
Uchaguzi huo uuliandaliwa na Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC baada ya aliyekuwa Mjumbe wa wadi hiyo Ronald Sagurani kuaga dunia mwezi Agosti mwaka wa 2021.