Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Pwani, Dogo Richie ameendelea kugonga vichwa vya habari za burudani baada ya kufichua kwamba anamchukia Ringtone kwa kile alichokitaja kama kuingilia masuala binafsi ya watu na kuyaanika mitandaoni.
Akizungumza kwa mahojiano na kituo kimoja cha habari jijini Nairobi, Richie alieza kuwa mashabiki wanahitaji muziki wake zaidi kuliko kiki anazozifanya mitandaoni.
Mwanamuziki huyo ambaye sasa hivi yupo chini ya usimamizi wa Kaya Records Kenya, alieleza kuwa kuna mipango mingi kutoka kwa usimamizi wake mpya ya collabo na wasanii wakubwa Afrika.
Aidha, Richie alisema kwamba anakubali ngoma za Khaligraph Jones. Richie alipoulizwa kuhusu Otile Brown alimtaja kama mpambanaji, Masauti kuwa ana roho safi na B Classic kama mwenye bidii.
Richie ambaye anazidi kutamba kwa ngoma yake ya kwanza kuiachia chini ya label yake ya Kaya Records Kenya, alipakia video ya wimbo huo kwenye mtandao wa Youtube, saa tatu asubuhi, siku ya jana.
#Uhondo #DogoRichie #Ringtone #KhaligraphJones #Masauti #OtileBrown #BClassic #EntertainmentNews #CelebrityUpdates