Picha kwa Hisani –
Mwanamuziki matata kutoka mkoa wa Pwani, Dogo Richie, ambae amepata umaarufu kwa hulka yake ya kuwachamba wanasiasia na wasanii wenzake kwa ngoma zake, alialikwa kwenye tamasha la kiserikali kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu sanaa. Inakadiriwa kuwa hali hii imetokana na tabia yake ya kuwakosoa wanamuziki wenzake.
Juzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kuwekwa benchi na waandaji wa matamasha haswa kwenye jimbo la Mombasa, Dogo Richie alipanda jukwaani kwenye tamasha la kusherehekea siku ya utalii duniani. Kwa hamu na gamu mashabiki walisubiri kufika kwa zamu ya nyota huyu wa muziki.
Dogo Richie alipo panda jukwaani mashabiki walipagawa na kuimba nyimbo zake zote alizoimba kwenye jukwaa.