Mwanamuziki wa nyimbo za kizazi kipya kutoka Pwani ya Kenya, Dogo J, amefichua kujaliwa mtoto wake wa kwanza miezi mitatatu iliyopita. Dogo J ambaye ni maarufu kwa wimbo wake ‘Napambana’ alieleza furaha yake baada ya kujaliwa mtoto wa kike, kupitia ujumbe aliouchapisha kwa status zake za WhatsApp.
Msanii huyo alilitaja jina la mtoto huyo kuwa Elizabeth na kusema kuwa ameona wakati huu kama mwafaka wa kumtambulisha mtoto wake kwa mashabiki wake. Dogo J pia alimpongeza mke wake kwa kumletea mtoto Elizabeth na kuelezea upendo wake kwake.
Aidha, mwanamuziki huyo pia hakusita kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumwombea mtoto wake maisha marefu yenye furaha. Dogo J alifichua kuwa huenda akamwimbia Elizabeth wimbo ili kueleza furaha yake.
Hata hivyo, Dogo J hakufichua mama mtoto ambaye ni mke wake.