Picha kwa hisani –
Huenda shule zikasalia kufungwa kutokana na kushuhudiwa kupanda kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini hadi hali itakapokuwa shwari licha ya wanafunzi wa gredi ya nne, darasa la nane na kidato cha nne kuruhusiwa kurudi shuleni.
Katibu mkuu msimamizi katika Wizara ya Afya nchini Dkt Mercy Mwangangi amesema hali kwa sasa sio salama kwa watoto kuruhusiwa kurudi shuleni, kwani bado kuna changamoto za kudhibiti msambao wa virusi vya Corona.
Akizungumza baada ya Kongamano la kudhibiti Corona, Dkt Mwangangi amesema ni lazima wakenya wazingatie masharti ya kujikinga na virusi hivyo hasa kwa kuvaa barakoa, kuosha mikoni kila mara, kutumia viezi na kukaa umbali wa mita moja kutoka wa wengine.
Wakati uo huo amewahimiza wazazi kuhakikisha wanaridhia juhudi za serikali za kupambana na janga la Corona na wala sio kuishinikiza kuzifungua shule ilhali hali ya kiafya kwa wanafunzi bado sio salama.