Story by Mwahoka Mtsumi –
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Afya nchini Dkt Patrick Amoth ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi kuu ya Shirika la afya duniani WHO kushikilia nafasi hiyo na kuhudumu katika makao makuu ya shirika hilo jijini Geneva.
Tangazo hilo la uteuzi wa Dkt Amoth limetolewa na mtangulizi wake Dkt Harsh Vadhan, katika mkutano wa 119 wa bodi hiyo ya Shirika la WHO.
Bodi hiyo kuu ya WHO, inajumuisha wanachama 34 huku kiongozi wa bodi hiyo akichaguliwa kwa kuzingatia misingi ya usawa wa nchi na kwa kuthmini mtu mwenye tajriba ya maswala ya kiafya.
Hata hivyo Wizara ya Afya nchini imepongeza uteuzi huo ikisema Dkt Amoth anatajriba ya kutosha kushikilia nafasi hiyo.