Story by Mwanaamina Fakii-
Naibu Katibu mkuu msimamizi katika Wizara ya Afya nchini Dkt Rashid Aman amesema Wizara hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya hadi mashinani kwani ni kati ya mpango wa ajenda nne kuu ya serikali.
Akizungumza katika Kongamano la Wanafamasia nchini inaloendelea katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, Dkt Aman amesema iwapo wanafamasia wataboresha utendakazi wao basi wananchi mashinani watanufaika na huduma za afya.
Dkt Aman hata hivyo amedokeza kwamba usalama wa wagonjwa upo mikononi mwa wanafamasia hivyo basi ni sharti madaktari hao waboreshe taaluma zao katika kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa.
Kwa upande Afisa wa afya anayesimamia maswala ya upangaji uzazi katika Wizara ya Afya nchini Dkt Issak Bashir amependekeza maafisa wa afya wa nyanjani kupewa mafunzo zaidi ili kuwawezesha kutoa huduma bora za upangaji uzazi kwa wananchi.