Story by our Correspondents-
Wizara ya afya nchini imesema inalenga kuongeza idadi ya watu wanaochangwa chanjo ya Corona kutoka watu elfu 80 hadi watu elfu 150 kwa siku kabla ya mwezi Disemba mwaka huu.
Mwenyekiti wa Jopokazi la utoaji wa chanjo ya Corona nchini Dkt Willis Akhwale amesema Wizara hiyo ina mipango ya kuongeza vituo vya kuwachanja wananchi kutoka vituo 800 hadi elfu tatu.
Dkt Akhwale amesema kufikia mwezi Septemba mwaka huu Kenya inatarajia kupokea dozi milioni mbili aina ya Pfizer, dozi elfu 390 ya Johnson na Johnson, dozi elfu 700 ya AstraZeneca, dozi zengine milioni mbili ya Sinophirm na dozi elfu 880 ya Moderna.
Hata hivyo amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi na kuchanjwa ili kupata kingi zaidi ya mwili ya kupambana na maambukizi ya Corona, huku akisema Wizara ya Afya nchini itafanya kila juhudi kuhakikisha wananchi wanapata chanjo.