Picha Kwa Hisani – Diana B
Msanii mpya kabisa wa mtindo wa kufoka kwenye tasnia ya muziki nchini Diana B ameachia ngoma mpya ambayo amemshirikisha Vinny Flava kwa jina ‘Mubaba’ kwenye mtandao wa Youtube.
Hii inakuja siku chache baada ya wawili hao kuibua madai kwamba akaunti ya YouTube ya msanii Diana B ilikuwa imezamishwa na mtu asiyejulikana.
Madai hayo yalikuwa yanasema kuwa kando na mtu huyo asiyejulikana kuizamisha akaunti hiyo, pia alifuta kila kitu kilichokuwepo na kuibadilisha jina kabla ya kuifuta.
Lakini baadae wakenya walidadisi na kuibuka na habari kinzani kwamba akaunti hiyo haikuwa imezamishwa na mtu asiyejulikana bali ni wawili hao waliifunga kwa muda tu ili kuvutia wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii.
Picha Kwa Hisani
Ikumbukwe Diana B alikuwa anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya siku moja tu kabla ya kuzua madai hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram.