Baada ya kupigwa kibano cha kutofanya maonyesho ndani na nje ya Tanzania sasa msanii wa Bongo Flava Diamond Platinumz amenyenyekea na kuomba msamaha.
Diamond na Rayvanny wameomba msamaha kwa serikali kwa kosa la kucheza wimbo wa Mwanza katika tamasha la Wasafi.
Haya yanajiri huku mpenzi wa zamani wa Diamond, Wema Sepetu akililia BASATA kumwondolea marufuku iliyomwekea kwa kupachika picha chafu mtandaoni.
Diamond amepangiwa tamasha kubwa humu nchini jambo linalozua ati ati kufuatia marufuku aliyopewa.
Taarifa na Dominick Mwambui.