Taarifa na Sammy Kamande.
Mombasa, Kenya, Julai 17 – Jamaa mmoja amefikishwa katika mahakama ya Shanzu kwa madai ya kumdhulumu mwanafunzi wa darasa la nane.
Mahakama imeelezwa kuwa Fredrick Mungai Njenga ambaye ni mhudumu wa magari ya uchukuzi ya Uber amefikishwa mahakamani kwa madai ya kumlazimisha mtoto mvulana mwenye umri wa miaka 13 kumnyonya sehemu yake ya siri mnamo Julai 15 mwaka huu eneo la Bombolulu kaunti ya Mombasa.
Aidha hakimu Yusuf Shikanda hakumsomea mshukiwa kesi inayomkabili na kusema shtaka aliloandikiwa halikuambatana na tendo analodaiwa kufanya na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja au pesa taslim shilingi elfu 50.
Kesi hiyo itaendelea tarehe 23 Julai mwaka huu ambapo mshukiwa atasomewa mashtaka yanayo mkabili.