Waziri wa fedha nchini Henry Rotich amesoma bajeti ya kitaifa ya shilingi trilioni 3 kwa ajili ya matumizi ya mwaka wa kifedha 2019/2020.
Akisoma bajeti hiyo waziri Rotich amesema kuwa deni la taifa ambalo kwa sasa limefikia shilingi trilioni 5.3 linadhibitiwa,huku akizitaka serikali za kaunti kutoidhinisha miradi mipya badala yake kukamilisha miradi ilioanzishwa hapo awali.
Katika bajeti hiyo Rotich amesema shilingi bilioni 326 zimetengewa idara ya usalama huku bilioni 2.9 zikitengewa taasisi za kupambana na ufisadi nchini ikiwemo tume ya EACC na afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma ili kufanikisha vita dhidi ya ufisaidi.
Shilingi bilioni 450.9 zimetengewa mpango wa agenda nne kuu za serikali,shilling bilioni 314 zikielekezwa kwa serikali za kaunti kote nchini huku idara ya nyumba ikitengewa shilingi billion 10.5.
Katika sekta ya elimu shilingi bilioni nne zimetengwa kugharamia ada za mitiani ya kitaifa ya KCPE na KSCE kwa wanafunzi wa humu nchini huku shilling billion 3.2 zikitengwa kuajiri waalimu zaidi, sekta ya afya ikitengewa kima cha shilling billion 47.8.
Vile vile awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR umetengewa billioni 55.5, hazina za vijana,wanawake na watu wanaoishi na ulemavu ikitengewa bilioni moja huku sekta ya michezo na sanaa ikitengewa shilingi bilioni 7.9.