Picha Kwa Hisani –
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa, Mwanamuziki kutoka Pwani Dazlah Kiduche amefichua mipango yake ya kuzindua kibao chake kipya hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa FaceBook, msanii huyo amesema kuwa yeye ndiye ‘Best show perfomer’ kati ya wasaani wanaotoka pwani na hivi karibuni anarudi kuchukua nafasi hio.
“#thefuture nimesikia kelele nyingi sana mengi yamesemwa. Mwisho wa Kwisha naitaka nafasi yangu I’m still the best performer and show killer in Coast and I’m about to bring you #worldwidehittracks only keep subscribing to my YouTube channel.” – aliandika Dazlah.
Dazlah ambaye alikuwa amepotea kwenye tasnia ya burudani kwa muda tangu alipositisha kufanya kazi na Producer Tee Hits amewaambia mashabiki wake kuwa wawe tayari kupokea hits kali ambazo anapanga kuchia hivi karibuni.