Post ya nyota wa muziki kutoka hapa Pwani Davy Gze imezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii.
Davy Gze ametangaza kuachana na kazi za sanaa ya muziki katika post hiyo aliyoichapisha kupitia ukurasa wake wa Facebook na caption inayosomeka hivi;
“Moyo wangu bikra ukiugusa tu unatoa damu ….Leo na surrender siwaezi kimziki…” Aliandika Gze.
Ni jambo ambalo limewachanganya mashabiki zake japo kufikia sasa hajataja hasa chanzo cha kufikia uamzi huo.
Kutokana na caption yake ni wazi kuwa, rapa huyo anapitia changamoto flani kwenye sanaa ya muziki.
Aidha, Gze ameonekana kutambua kazi za marapa wenzake Sudi Manjewayne na Deno Mkali.
“…ila tambueni mkimtoa Sudi Manjewayne na Deno Mkali hakuna rapper mwengine wakunitisha 😜,sema tu ni vile niliacha mziki.” Aliandika Davy Gze
Ikumbukwe kwamba huyu sio msanii wa Kwanza kutoka Pwani ya Kenya kusitisha safari yake ya muziki, juzi kati pia msanii Dully Melody alitamka kuacha muziki.
Je unahisi tatizo liko wapi?